Kocha wa Manchester United, Jose Mourihno yuko mbioni kumnasa winga wa klabu ya genk na timu ya taifa Tanzania, mbwana samatta
Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 1 Aprili Jose Mourihno amethibitisha kuvutiwa na winga huyo wa Yanga mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na kila kitu kipo kwenye hatua zamwisho ili kuipata saini ya nyota huyo
"Ni kweli tumekuwa tukimfuatilia Samagoal kwa muda mrefu sasa, mawakala wetu walikuwapo Tanzania wiki hii ili kumalizana na klabu ya genk kuhusu dili hilo. Natumaini leo tarehe moja Aprili samatta atakuwa ni mali halali kwetu.
"Kikubwa kasi yake uwanjani, uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na pia kufunga ndiyo sababu kubwa kwetu kumsainisha samatta, natumaini ataongeza ubora kwenye timu yetu hasa kwenye eneo la ushambuliaji ambalo lina upungufu mkubwa tangu ibrahimovic aumie, alisema kocha huyo wa Man United, Mreno Jose Mourihno.
"Tarehe kama ya leo ni nzuri sana kwangu kwani ni siku ambayo naweza sajili mchezaji yoyote yule duniani nimtakaye", alimalizia Mourinho
Samatta anatarajiwa kuondoka leo tarehe moja Aprili kuelekea Uingereza kwa ajili na kujiunga na Manchester United rasmi.
Watanzania kwa ujumla wako nyuma yake kwa ajili ya kumtakia mafanikio mema kwenye safari yake ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
ConversionConversion EmoticonEmoticon