Nahodha wa Azam FC John Bocco, amesema wapo fiti kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Mbabane Swallows, katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopangwa kupigwa Jumapili Uwanja wa Azam Complex.
Bocco anasema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaitoa timu hiyo na kutinga hatua ya makundi , na hatimaye kucheza fainali ya michuano hiyo kwa mwaka huu.
“Unajua kwa sasa tupo vizuri ukilinganisha na mwanzoni mwa msimu, hilo ndiyo linatupa matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka huu, kwa sababu tuna kikosi kizuri na kocha mwenye uzoefu na mashindano kama haya,” amesema Bocco.
Nahodha huyo amesema pamoja na kutowajua vizuri wapinzani wao Mbabane Swallows, lakini anaamini mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani, ingwa anaamini wataibuka na ushindi baada ya dakika 90 za mchezo huo.
Amesema mipango yao ni kutaka kutimiza malengo ya kufika mbali kuliko awamu zote walizowahi kushiriki michuano ya kimataifa na kujiwekea rekodi ya pekee wakiwa kama timu ngeni kwenye soka la Tanzania.
Azam inayofundishwa na kocha Aristică Cioabă, imepangwa kuanza raundi ya kwanza michuano hiyo baada ya mwaka jana kutolewa raundi ya pili kufuatia kutolewa na Esperence ya Tunisia.
Hii ni mara ya nne kwa Azam kushiriki michuano ya kimataifa na mara moja ilikaribia kutinga hatua ya 16, bora lakini akatolewa na FAR Rabat ya Algeria.
ConversionConversion EmoticonEmoticon