Google translator

MASHETAN WEKUNDU WANG'ARA UEROPA


Huku wakiwa barazani kwao mashetani wekundu maarufu kama 'the red devils' usiku wa jana wameihadhiri feyernood ya uholanzi kwa ushindi wa bao 4 bila majibu,shukran kwa wayne rooney aliyefunga goli moja na kuikaribia rekodi ya kufunga magoli mengi united inayoshikiliwa na sir.boby charlton aliyefunga mabao 249 ambapo anamzidi rooney aliyeweka wavuni mara 248.Magoli mengine yaliwekwa wavuni na zlatan ibrahimovic,juan mata na winga chipukizi jesse lingard aliyefunga bao safi kufuatia gonga iliyopigwa na wachezaji wa united.
katika wakati mwingine kiungo hatari wa mashetani hao henrikh mkhitaryan amerudi vyema dimbani mara baada ya jana kupiga mpira mwingi sana na kuwa man of the match katika pambano hilo licha ya kukosa magoli mengi ya wazi na hii imepelekea kocha josse mourinho kuahidi atampanga katika mechi ijayo dhidi ya wagonga nyundo wa london westham united jumapili katika dimba la old trafford 'machinjioni'

Previous
Next Post »