Mlinzi wa kati wa Yanga SC Kelvin Yondani, ataikosa mechi ya kesho dhidi ya MC Alger katika play- offs ya kombe la shirikisho kuwania nafasi ya makundi .
Kocha msaidizi wa Yanga SC akiongea na waandaaji wa kipindi cha Yanga SC TV Online amethibitisha hilo pia akielezea nafasi yao katika mchezo huo muhimu. " tumejipanga vyema kushinda mchezo wa kesho licha ya majeruhi tulionao kikosini . Yondani kaumia mazoezini hivyo anaweza ukosa mchezo huo , Ngoma ameanza vyema mazoezi lakini kama ilivyo kwa Kamusoko wanakosa match fitness. Tambwe nae bado hajarudi vizuri katika hali yake sambamba na Justine Zulu aliyeshonwa juzi sita juzi .
Vijana waliobaki wana hali nzuri kuicheza mechi hiyo na morali yao , uelewa wa mazoezi hakika unatupa matumaini hapo kesho " alieleza kocha huyo anaesifika kwa kuwajenga wachezaji kisaikolojia na fiziki.
Tayari timu ya MC Alger imeshawasili tangu jana usiku nchini kwa ndege ya kukodi na leo watafanya mazoezi katika uwanja wa taifa kuelekea mchezo huo wa kesho.
ConversionConversion EmoticonEmoticon