Google translator

BREAKING NEWS:PLUIJM ASAINI SINGIDA UNITED

TIMU ya Singinda United imegoma kuthibisha kuwa imemalizana na kocha Hans van der Pluijm lakini ni wazi huyo ndiye kocha mpya wa kikosi hicho kilichopanda kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
Mkataba wa Pluijm, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Yanga ulivunjwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa klabu hiyo imeshindwa kumlipa mholanzi huyo aliyeipa mafanikio makubwa Yanga wakati akiwa kocha mkuu.
Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima amesema, suala la Pluijm litatolewa taarifa kama lipo au halipo.
“Maana ni mazungumzo ya awali yamefanywa ila hatuwezi kutamka kuwa ni kocha wetu wakati hatujamalizana naye litakuwa si jambo la busara,” Sima
Aidha katibu Sima alisema kuwa: “Tutaangalia taarifa na uhitaji wa benchi la ufundi hapo baadaye, muda wa kufunguliwa kwa usajili wetu bado.”
Kutokana na urafiki uliopo kati ya Pluijm na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ndio kunapelekea watu kuhisi huenda Pluijm akatua Singida United timu ambayo ipo karibu na Mh. Nchemba.
Previous
Next Post »