Vinara wa ligi kuu ya vodacom tanzania bara simbasc ipo mbioni kukamilisha usajili wa golikipa kutoka ghana anayekipiga medeama fc Daniel Agyei.Akithibitisha hilo ofisa habari wa simbasc Hajji manara kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii wa twitter amesema ni kweli agyei anakuja msimbazi kutokana na tetesi zilizosambaa katika kipindi kifupi na sasataarifa hizo zimekuwa rasmi.
Agyei anakuja simbasc kumpa changamoto vicent angban raia wa ivory coast ambaye ndiye kipa namba moja msimbazi hivyo anatarajiwa kutua jumatano kukamilisha dili hilo na tayari amekwisha waaga wachezaji wenzake pamoja na viongozi wa medeama kuwa anaondoka kupitia akaunti yakew ya facebook.
Agyei ndiye kipa namba mbili wa timu ya taifa ya ghana na anatarajiwa kuja dsm kwa mara ya pili mara baada ya kutua bongo mara ya kwanza akiwa na klabu yake ya medeama fc kucheza dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa makundi ligi ya shirikisho barani Afrika,mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1 na katika mechi hiyo Agyei aliikosesha ushindi yanga mara baada ya kuokoa michomo mingi iliyoletwa langoni ,mwake.
ConversionConversion EmoticonEmoticon