Google translator

UNITED NA SO'UTON ZATINGA NUSU FAINALI EFL CUP



Klabu ya soka ya manchester united imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la ligi maarufu kama EFL CUP mara baada ya kushinda goli 4-1 dhidi ya wagonga nyundo wa london westham united.

United ndo walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa z.ibrahimovic aliyeweka kambani mara mbili dk.2 na dk.90+3 huku mengine yakiwekwa nyavuni na antony martial dk.48 na dk.62.westham walijipatia goli la kufutia machozi kupitia fletcher dk.35 ya mchezo.

 Katika pambano jingine Arsenal imekula mweleka baada ya kufungwa goli 2-0 dhidi ya southampton shukrani ziende kwa Jordy classie dk.13 na Ryan betrand dk.36.
Jordy classie akishangilia goli na wenzake 

Pia katika mechi hiyo timu zote zilisimama kjmya kwa dakika moja kuomboleza vifo vya wahanga wa ajali ya ndege iliyotokea colombia siku ya jumatatu.


Previous
Next Post »