Google translator

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA BRAZIL YAPATA AJALI

Ndege iliyokuwa imebeba watu 81 ikiwemo baadhi ya wachezaji wa klabu ya soka ya chapecoence ya brazil na abiria wengine imepata ajali nchini colombia.Ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini medellin  ambapo wachezaji wa chapecoence walikuwa wakiwahi mechi ya fainali mkondo wa kwanza kombe la copa sudamericana dhidi ya club atletico nacional siku ya jumatano.Habari zisizo rasmi kutoka katika chombo kimoja cha habari nchini hispania kimesema wachezaji wawili wamenusurika ambao ni allan ruschel na danilo lakini wengine bado haijajulikana hatma yao.
                                                                      Wakati huohuo Shirikisho la soka amerika ya kusini limesimamisha mechi hiyo mpaka habari rasmi zitakapotoka  kuhusiana na ajali hiyo lakini chanzo kikubwa cha ajali hiyo inasemekana ni kuchafuka kwa hali ya hewa na uzuri haikuungua na moto hivyo kuna mategemeo ya majeraha wengi.
Previous
Next Post »