Klabu ya soka ya liverpool imeshinda magoli 2-0 dhidi ya leeds united kwenye EFL CUP katika pambano lililopigwa katika dimba la anfield.Magoli hayo yaliwekwa nyavuni na straika divock origi dk76 na ben woodburn dk81
.
Kivutio katika pambano la jana ni goli lililofungwa na dogo kutoka wales ben woodburn aliyevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi liverpool kufunga goli katika timu ya wakubwa,rekodi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na mchezaji wa zamani wa liverpool na timu ya taifa ya england michael owen.
Akielezea kupitia account yake katika mtandao wa kijamii wa twitter owen amesema''hongera kwa ben woodburn ambaye amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga goli liverpool akiwa na umri wa miaka 17 na siku 45''.Dogo huyo anavunja rekodi hiyo kwa tofauti ya siku 98 ambapo owen alifunga goli lake la kwanza liverpool akiwa na umri wa miaka 17 na siku 143.Trent alexander dogo mwingine wa loverpool akifurahi na mwenzake Woodburn. |
ConversionConversion EmoticonEmoticon