Google translator

WAWA AIKACHA AZAMFC ARUDI MERREIKH

Beki kisiki wa azamfc serge pascal wawa ameamua kuachana na mabingwa hao wa kagame cup msimu ulopita na kutimkia kwa matajiri wa sudan el merreikh mara tu mkataba wake utakapoisha mwaka huu.Hii inakuja mara baada ya kocha mkuu azamfc zeben hernandez kusema kuwa hana nafasi katika kikosi chake kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya mchezaji huyo hivyo kutimkia merreikh.Kwa upande wake wawa amesema chaguo la kwanza lilikuwa azamfc lakini kutokana na yeye kutohitajika ameamua kusaini merreikh kwani ni sehemu bora zaidi kwa kiwango chake kwani sudan kuna ligi bora kulinganisha na Tanzania lakini pia anaweza kufika mbali katika ligi ya mabingwa afrika tofauti kama angekuwa azamfc.
wawa akipewa tuzo ya mchezaji bora wa mechi kagame cup.
       serge wawa hatosahaulika azamfc pia Tanzania kwa ujumla kutokana na uwezo wake wa hali yajuu katika kuzuia mashambulizi ya timu pinzani mpaka kupewa  jina la waziri wa ulinzi.KILA LA KHERI PASCAL WAWA HUKO UENDAKO.                                                                                                                                                 
Previous
Next Post »