Google translator

HUYU NDIYE MTANZANIA ANAYEKINUKISHA BUNDESLIGA

Yussuf poulsen ni mshambuliaji wa kimataifa wa denmark na klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi kuu nchini ujerumani maarufu kama bundesliga,mchezaji huyo ana asili ya tanzania aliyezaliwa mwaka 1994 katika mji wa coppenhagen nchini denmark ambapo mama yake akiwa ni raia wa denmark huku baba yake akiwa ni mtanzania.Baba yake alikuwa ni mfanyabiashara aliyefariki mwaka 2000 ambapo yussuf alikuwa na umri wa miaka sita tu.Ni mchezaji aliyeichezea denmark kwenye ngazi zote za vijana na mpaka timu ya wakubwa ambapo aliitwa mara ya kwanza katika mbio za kufuzu euro 2016 baada ya kuwasha moto katika timu za vijana.

Previous
Next Post »