Kiungo wa klabu ya zesco united na timu ya taifa ya zambia Justine Zulu ametua uwanja wa kimataifa wa mwl.J.K.Nyerere Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.Zulu anakuja dsm kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na mabingwa wa soka tanzania Young africans.kuna uwezekano mkubwa wa kiungo huyo mkabaji kumwaga wino jangwani kwani ni pendekezo la kocha mkuu wa timu hiyo george lwandamina.Mchezaji huyo atakutana na uongozi wa yanga siku ya leo wakiongozwa na mwenyekiti yussuf manji
Zulu anakuja yanga kutokana na tatizo la kiungo mkabaji hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa kiraka kutoka Congo DRC bwana mbuyu twite kutemwa kutokana na sheria za ligi kuu ya vodacom kwa wachezaji kutoka nje ya nchi hivyo yanga itakuwa imetimiza wachezaji nane na mmoja lazima akatwe ili wabaki wachezaji saba wa kigeni na twite ndo mtu sahihi kwani ameshindwa kucheza vizuri kama kiungo mkabaji.

ConversionConversion EmoticonEmoticon