Google translator

ARSENAL YAFANYWA VIBAYA GOODSON PARK

Ashley williams akishngilia bao lake dhidi ya arseanal.

Washika mitutu wa jiji la london arsenal wamefungwa magoli mawili kwa moja dhidi ya everton kwenye mechi ya ligi kuu nchini uingereza iliyofanyika uwanja wa goodson park.Arsenal ndio walianza kufunga bao kupitia kwa mshambuliaji wao tegemezi alexis sanchez dk.20

Hata hivyo goli hilo likaruda dk.44 kupitia kwa mlinzi wa everton seamus coleman mara baada ya kuunganisha krosi safi kutoka kwa full beki wa kushoto leighton baines na kuruka juu zaidi huku akiwaacha mabeki wa arsenal wakishangaa..



Kipindi cha pili kilinza kwa kasi kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu lakini dk.86 beki wa kimataifa wa wales ashley williams  aliifungia klabu yake ya everton goli la pili kwa kichwa safi tatizo jingine la kushindwa kujipanga kwa mabeki wa arsenal na yeye bila ajizi aliweka mpira huo kambami na mpaka mwisho arsenal walitota kwa magoli 2mawili kwa moja.

Katika pambano jingine Afc bournemouth wameshinda goli moja kwa bila dhidi ya leicester city,shukrani ziende kwa  marc pough aliyefunga goli hilo.




Previous
Next Post »