Google translator

OMOG AIPAISHA SIMBASC

Omog akiwa kazini uwanja wa taifa ligi kuu bara msimu huu.


Kocha mkuu wa klabu ya soka ya simbasc joseph omog ameitetea timu yake ya simbasc klabu kuwa ilifungwa bahati mbaya hapo jana dhidi ya wakata miwa wa mtibwa sukari ya mjini morogoro.mechi hiyo iliisha kwa simbasc kupigwa goli mbili kwa moja pale chamazi mbande jijini dar es salaam yalipo makazi ya azamfc.

Omog amenukuliwa na mtandao wa michezo wa saddie blog akisema kuwa amegundua baadhi ya makosa kwenye mechi ya jana ikiwemo kukatika kwa beki ya kati ya simbasc lakini atayafanyia kazi makosa hayo hivyo mashabiki wa msimbazi wasiwe na presha na timu yao.

Aidha omog ameongeza kuwa timu yake itatwaa ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu na kuwapiku watani wao yangafc waliobeba kombe hilo msimuu uliopita.

Ligi kuu bara itaendelea wikiendi hii ikiwa ni mzunguko wa pili ambapo simbasc itasafiri mpaka mtwara kuwavaa ndanda kuchere nyumbani kwao mara baada ya kushinda gemu ya kwanza uwanja wa taifa kwa magoli 3 dhidi ya 1 la ndandafc.

Previous
Next Post »