Haya ndo majembe matatu maapya azamfc yakitambulishwa na kocha zeben hernandez |
Matajiri wa ligi kuu ya vodacom (VPL) azamfc leo imeua ndege watatu kwa mpigo mara baada ya kusainisha majembe matatu mapya kutoka ndani na nje ya nchi.Wawili wanatoka nje ya nchi ambao ni Stephan kingue mpondo kutoka cotton sports ya cameroon na Yakub Mohammed kutoka Aduana stars ya Ghana.mwingine ni winga Joseph mahundi aliyetokea mbeya city ya jijini mbeya.
Mpondo ni kiungo mkabaji maarufu kama ''mkata umeme'' aliyeiongoza cameroon kwenye chan mwaka huu amesaini mkataba wa miaka mitatu na anakuja kuziba pengo lililoachwa na jean mugiraneza ''miggi'' aliyeimkia vietnamm.
Yakub mohammed (20) ni beki wa kati aliyesaaini mkataba wa mwaka mmoja na anakuwa mghana mwingine kutua azam akitokea Aduna stars Ghana kuja kuziba pengo lililoachwa na pascal wawa aliyetmkia merreikh.
Joseph mahundi naye amesaini mkataba wa miaka miwili na anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji azamfc
ConversionConversion EmoticonEmoticon