Costa akishangilia bao lake dhidi ya crystal palace. |
vinara wa ligi kuu uingereza chelsea ''the blues'' wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifumua crystal palace ugenini.chelsea imepata ushindi wa bao 1-0 lililowekwa nyavuni na straika wao tegemezi diego costa dk.44 kufuatia krosi safi ya beki wa kulia cesar azpilicueta.
Hadi sasa chelsea imecheza mechi 17 ikishinda mechi 14 ikidroo 1 na kufungwa mechi 2 hivyo inafikisha pointi 43 mbele ya liverpool na arsenal zenye pointi 34.
Hata hivyo chelsea itawakosa wachezaji wake muhimu straika diego costa na kiungo ng'olo kante kwenye mechi ijayo dhidi ya bournemouth siku ya boxing day kufuatia kupewa kadi mbili za njano.
ConversionConversion EmoticonEmoticon