Google translator

KASEJA AMWAGA WINO TIMU LIGI KUU


Klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu tanzania bara kagera sugar imemnasa golkipa juma kaseja kutoka mbeya city ya mkoani mbeya.Mratibu wa kagera sugar amethibitisha ujio wa kaeja katika timu yao na tayari amekwishaanza mazoezi na timu kujiandaa na mzunguko wa pili ligi kuu ya vodacom VPL.

Kaseja ambaye ni golkipa namba moja wa zamani wa timu ya taifa ''Taifa stars'' anakuja kagera sugar akitokea mbeya city ambayo amemaliza nayo mkataba na kujiunga na kikosi kipya kinachofundishwa na mzawa mecky mexime huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga na wakata miwa hao.

Aidha uongozi wa kagera sugar umepanga kuachana na kipa wake Mohammed sharrif ''casillas'' baada ya kumfungia kucheza katika timu hiyo kutokana na madai ya kuuza mechi dhidi ya yanga waliyopigwa magoli 6-2 katika uwanja wao wa kaitaba mkoani kagera.
Previous
Next Post »