Google translator

MOURINHO AFUNGUA MILANGO UNITED



Kocha mkuu wa manchester united josse mourinho amefungua milango kwa wachezaji wanaotaka kuihama klabu hiyo.Mourinho amesema hayo baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi za kuhama juu ya mastaa mbalimbali wanaokipiga klabuni hapo.

Mourinho ameeleza kuwa ana furaha na kikosi alichonacho mpaka mwisho wa msimu,sikuwahi kumfuata mchezaji yeyote na kumwambia kuwa sikutaki katika kikosi changu ila kama itatokea kuna mtu anataka kuondoka ili mradi timu itakayomhitaji itimize matakwa yetu ikiwemo na dau litakalotushawishi.

Moja ya wachezaji wanaohusishwa na kuondoka united ni winga wa kimataifa wa uholanzi memphis depay (22) anayewaniwa na vilabu vya as roma ya italia na everton ya nchini uingereza,na hii inatokana na kukosa namba mara kwa mara tangu mourinho atue old trafford.


Depay ameichezea united mechi 53 tangu atue klabuni hapo huku akiweka kimiani mabao 7 tu.Mara ya mwisho depay kuanza kikosi cha kwanza ni kwenye mechi ya EFL CUP ambapo unites walicheza na Northampton fc.

Wachezaji wengine wanaohusishwa na kuondoka united ni pamoja na kiungo mkabaji morgan schneirderlin,bastian schweinsteiger na beki wa kushoto luke shaw aliyekataa kujiunga na chelsea mwaka 2014 akitokea southapmton fc na kuwachagua mashetani wekundu.

Wakati huohuo man utd inasemekana ipo mbioni kumuwania mshambuliaji wa atletico de madrid Antoinne Griezmann kutokana na tatizo la kutokuwepo kwa mshambuliaji atakayekuja kubadilisha mchezo pale united inapozidiwa.

Previous
Next Post »