Google translator

NI POGBA VS POGBA UEROPA LEAGUE

Florentin pogba na paul pogba.



Mara baada ya ratiba ya kombe la ueropa league kutoka leo hii,mjadala mkubwa ni pambano baina ya mashetani wekundu manchester united vs st.ettiene ya huko ufaransa.

Katika mechi hiyo watakutana ndugu wawili wenye asili ya africa ambao ni paul pogba na ndugu yake florentin pogba.Florentin pogba ni kaka wa paul pogba na anakipiga st.ettiene ya ufaransa nafasi ya beki huku mdogo wake paul akicheza kama kiungo mchezeshaji katika klabu ya man utd ya huko uingereza.


Tofauti ya wachezaji hawa ni mataifa wanayoyawakilisha ambapo florentin pogba aliyezaliwa mwaka 1990 akiichezea timu ya taifa ya guinnea huku paul pogba aliyezaliwa mwaka 1993 akiiwakilisha ufaransa kama timu yake ya taifa.







Previous
Next Post »