Google translator

BREAKING NEWS;RONALDO ATWAA BALLON D'OR KWA MARA YA NNE

\Ronaldo akifurahia tuzo yake aliyobeba usiku wa kuamkia leo.

Mshambuliaji wa real madrid ya hispania na timu ya taifa ya ureno cristiano ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.Tuzo hiyo inatolewa na jarida moja  la mchezo nchini ufaransa liitwalo football france.

Tuzo hiyo inakuwa ni ya nne kwa ronaldo katika carrer yake ya soka,na amewapiku wenzake lionel messi wa argentina aliyeshika nafasi ya pili huku antoinne griezman akishika namba tatu.akizungumza mara baada ya kutwaa tuzo ronaldo amesema ni furaha kwake kuona kazi anyoifanya kuwa inathaminika japo haikuwa rahisi kuwapiku wenzake mpaka kuibeba tuzo hiyo kwani nimefanya kazi kubwa.




Ronaldo ameisaidia klabu yake kutwaa champions league msimu uliopita pia timu yake ya taifa kutwaa euro champinshiop june mwaka huu.Aidha ronaldo amefunga jumla ya magoli 51 kwenye mechi 54  kwa mwaka 2016 huku akiifungia timu yake ya taifa magoli 13 mwaka huu.



Previous
Next Post »