Google translator

MCHUJO WA VIJANA U-15 NA U-17 WAANZA AZAMFC




Mkuu wa maendeleo ya soka la vijana azamfc Tom legg ameanza kazi ya kuchuja vijana walioibuliwa ktoka maeneo mbalimbali jijini dar es salaam jana.vijana waliohudhuria mchujo huo walikuwa 34 badala ya 46 waliotakiwa kufika chamazi kwa ajili ya kutengeneza combine ya mkoa kwa wale watakaofuzu kwenye mchujo huo.

Zoezi hilo litaendelea mpaka siku ya jumatano na siku ya alhamisi tom atataja majina ya wachezaji waliofuzu na kuungana na wengine kutoka mikoani ili kuingia kwenye mchujo wa mwisho pale chamazi hivi karibuni.

Mchujo huo unajumuisha vijana chini ya umri wa miaka 15 na 17 unaolenga kutengeneza timu  nzuri kabisa ya vijana ya azamfc pia kusaidia timu ya taifa la Tanzania kwa siku za usoni.

  '' KILA LA KHERI AZAMFC KATIKA ZOEZI HILO''
Previous
Next Post »