Kiungo mshambuliaji wa mashetani wekundu manchester united henrik mkhitaryan amesifiwa na kocha wake josse mourinho.sifa hizo zinatokana na kiwango alichokionyesha kiungo huyotangu arejee kutoka kwennye majeraha na kuisaidia united iliyokosa ushindi kwenye ligi kwa wiki kadhaa.
Magoli mawili aliyoyafunga kwenye mechi mbili tofauti moja ikiwa ya ueropa league dhidi ya zorya na nyingine ya ligi kuu dhidi ya spurs yanathibitisha ujio mzuri wa mkhitaryan kutoka kwenye majeraha.
Akimzungumzia micki kocha wa manchester united josse mourinho amemmwagia sifa kiungo huyo na kusema amekuwa mchezaji mzuri tangu arudi dimbani kwani anaonekana ana kiu ya kuonyesha uwezo wake na mwenye njaa ya mafanikio.
Hata hivyo mourinho aliendelea kusema kuwa micki ndiye mchezaji wa kuigwa kwa sasa pale united kwani anacheza vizuri na haleti visingizio tofauti na baadhi ya wachezaji wengine wanaosingizia pitch ama hali ya hewa inayowafanya wasicheze vizuri.
micki (27) ni raia wa armenia ambaye alitua united dirisha kubwa mwaka huu kwa ada ya paun 26m na atakaa nje kwa wiki mbili mara baada ya kuumia enka kwenye mechi ya ligi dhidi ya spurs wikiendi ilyopita ambapo timu yake ilishinda goli moja uwanjani kwao old trafford.
ConversionConversion EmoticonEmoticon