Leo kwenye ligi kuu uinereza litapigwa pambano la kufa mtu kati ya washika mitutu wa london arsenal watakapokiuma na manchester city iliyo chini ya pep guardiola.Man city ndiyo itakuwa nyumbani kuwakaribisha arsenal kwenye dimba la Etihad.
Utamu wa pambano hili unakuja pale ambapo mmoja kati ya timu hizi akipoteza basi atakuwa ameachwa na mwenzake kwani wanatofautiana kwa pointi moja tu.Arsenal ndio wapo juu kwa pointi 34 sawa na liverpool nyuma ya vinara chelsea wenye pointi 43 hivyo tofauti yao ni pointi 9,huku man city akiwa na pointi 33 nyuma ya timu tatu ambazo ni arseanal,liverpool na chelsea.
Utamu mwingine katika pambano hili ni vita inayoendelea kati ya sanchez aliye kwenye kiwango bora kwa sasa ulaya na sergio aguero ambaye wanafukuzana kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu ambapo mbio hizo zinaongozwa na straika wa chelsea diego costa mwenye mabao 13 akifuatiwa na sanchez mabao 12,zlatan ibrahimovic naye anatimiza mabao 11 mara baada ya kufunga mawili jana dhidi ya west brom halafu Aguero anakuwa wa nne kwa mabao yake 10 aliyofunga kwenye ligi hiyo.
Zifuatazo ni rekodi ya mechi sita zilizopita kati ya man city vs arsenal 'head to head' ;
Arseanl 3-2 man city
Man city 2-2 Arsenal
Arsenal 2-1 man city
Man city 0-2 arsenal
Arsenal 2-2 man city
Arsenal 3-0 man city
NOTE;Man city haijafungwa kwenye mechi 10 kati ya 11 ilizocheza msimu huu kwenye uwanja wao wa nyumbani,sasa tusubiri tuone kama rekodi hiyo itaendelea ama kuvunjwa..??
ConversionConversion EmoticonEmoticon