Google translator

HILI NDILO AGIZO LA FIFA KWA VILABU KUFUATIA AJALI YA NDEGE COLOMBIA


Neto ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza aliyesalia katika ajali iliyotokea wiki hii..

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeamuru mechi zote zitazochezwa wikiendi hii duniani kote lazima zikae kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kuwakimbuka wahanga wa ajali ya ndege iliyotokea colombia jumatatu ya wiki hii na kuuwa zaidi ya watu 70 wakiwemo wachezaji na viongozi wa chapecoense ya brazil.

Kikosi hicho kilichokuwa kikienda kucheza fainali ya kombe la copa sudamericana kwa mkondo wa kwanza nchini colombia dhidi ya atletico nacional ya huko,kilipata ajali na kupoteza wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza kilichocheza mechi ya nusu fainali isipokuwa mchezaji mmoja tu aitwaye Neto ndiye aliyeokoka na ajali hiyo pamoja na wenzake watano  kutokana na sababu tofauti.Hivyo kikosi kimebaki na wachezaji sita tu.

Katika wakati mwingine FIFA imeamuru wachezaji wote kuvaa beji nyeusi kwenye mikono yao  ikiwemo michezo ya champions league pamoja na europa league na hii ni kuonyesha sapoti yao kwa chapecoense kutokana na kuguswa na ajali hiyo.

''MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI''

''AMEEN''



Previous
Next Post »