Oscar akishangilia kwenye moja ya mabao yake akiwa chelsea. |
Kiungo mshambulizi wa chelsea ''The blues'' Oscar dos santos antarajiwa kuelekea china mwezi ujao kwenda kujiunga na shanghai SIPG ya nchini humo katika dirisha dogo la mwezi january.Dili hilo limekamilika kwa 90% mpaka sasa na Shanghai SIPG wameweka mezani dau la pauni milioni 52 na chelsea watakuwa wagumu kukataa dau hilo.
Oscar amekosa nafasi ya kucheza ligi kuu uingereza tangu september mwaka huu na endapo atatua shanghai ataungana na kocha wake wa zamani andreas villas Boas anayeifundisha timu hiyo mara baada kuchukua nafasi iliyoachwa na kocha Goran Errickson aliyefukuzwa.
Akizungumza na mtandao wa michezo nchini Brazil ''Globbo'' oscar amesema kwa aslimia 90 dili hilo limekamilika na ataondoka chelsea kwenye majira haya ya baridi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon