Vinar wa ligi kuu Tanzania bara simbasc imefanikiwa kumnasa kiungo fundi kutoka Ghana james Kotei.James amesajiliwa msimbazi mara baada ya kufuzu majaribio aliyokuwa akiyafanya na alikuwemo katika kikosi kilichocheza na mtibwa sugar jumatatu ya wiki hii na kuambulia kichapo cha magoli 2-1.
Kotei amesaini mkataba wa mwaka mmoja na anakuwa mchezaji wa pili kutoka Ghana kusajiliwa msimbazi mara baada ya kipa daniel agyei naye kutoka ghana kusaini msimbazi wiki chache zilizopita.
Aidha simba ipo katika mchakato wa kumchukua mshambuliaji wa Tanzania anayekiuma Zesco united ya Zambia kwa ajili ya kuisadia safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Juma Luizio akiwa uwanjani kuitumikia klabu yake ya zesco ligi kuu nchini zambia. |
Usajili huu unafanywa baada ya maamuzi ya kikao cha viongozi kilichofanyika jana na kinahaha kukamilisha sajili hizo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa plili ligi kuu bara jumamosi hii.
ConversionConversion EmoticonEmoticon