Google translator

KAPOMBE ATISHIA AMANI AZAMFC

kapombe akiwa mazoezini na wachezaji wenzake azamfc.


Wing back wa azamfc na timu ya taifa ya Tanzania shomari kapombe yupo mbioni kurudi dimbani kuelekea mzunguko wa pili ligi kuu bara.Kapombe aliyekosa duru la kwanza msimu huu kutokana na majeraha hivyo amekwishaanza mazoezi na timu yake ambayo ndiyo matajiri zaidi ligi kuu bara pia afrika mashariki na kati.

Akinukuliwa kutoka mtandao wa klabu yake kapombe amesema tayari anaendelea na mazoezi na wenzake pia mazoezi binafsi ambayo yanampa moyo wa kufanya vema zaidi na kurejesha kiwango chake.

Kapombe anatajwa kama mlinzi bora zaidi wa kulia tanzania baada ya msimu uliopita kuweka kambani magoli 11 na kuwazidi baadhi ya washambuliaji wa timu mbalimbali ligi kuu bara na kuchangia azamfc kushika nafasi ya pili ligi kuu ya vodacom msimu uliopita.
Previous
Next Post »